![Überschrift: Run-up to Kenyan elections
Schlagworte: Kenyan elections 2013, Clearance for presidential candidates
Wer hat das Bild gemacht: James Shimanyula
Wann und wo wurde es aufgenommen: 30.1.13 Kenyatta International Conference Cneter, Nairobi Kenya,
Was ist darauf zu sehen : Kenya's Independent Electoral Commission Chairman Issack Hassan [left] and his Deputy, James Oswago, scrutinize Presidential Candidate Raila Odinga's documents for clearance in Nairobi. Odinga leads The Alliance of Coalition for Reform and Democracy, CORD Party.
--> James Shimanyula hat die Rechte an DW übertragen](http://www.dw.de/image/0,,16561852_303,00.jpg)
Huku Wakenya wakiendela kusubiri kwa hamu
kubwa kumjua mshindi wa kura ya urais kufuatia uchaguzi wa Jumatatu,
wasiwasi unaongezeka baada ya kukwama kwa mfumo wa uwasilishaji matokeo
kwa njia ya elekroniki.
Kufuatia hitilafu hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC)
imesema kwamba inategemea sasa matokeo yatakayowasilishwa na wasimamizi
wa uchaguzi kutoka majimbo yote 290 kote nchini ili kuanza upya shughuli
ya kujumlisha kura za urais.
“Maafisa wetu wa usimamizi wa uchaguzi wanatarajiwa kuleta matokeo rasmi
wakati wowote kuanzia sasa. Tutaanza kutangaza matokeo rasmi kutoka
maeneo bunge yote 290 kuanzia hapo kesho”. Alisema Mwenyekiti wa IEBC,
Isaack Hassan, hapo jana jioni baada ya kukwama kwa mfumo wa kuwasilisha
matokeo kwa njia ya elektroniki.
Hassan amedokeza kwamba idadi ya kura za urais zilizoharibika au
kukataliwa zitajumuishwa na kura zote zilizopigwa ili kupata hesabu ya
asilimia ya kura kwa kila mgombea...

Wafuasi wa muungano wa Jubilee.
“Kwa mujibu wa katiba jaduali la matokeo litarekebishwa kuonyesha
asilimia ya kura kwa kila mgombea kuzingatia kura zilizopigwa.”
Ikiwa hilo litafanyika, inamaanisha kwamba hakuna mgombea atakayepata
asilimia 50 ya kura zote na hivyo kupelekea kufanyika kwa duru ya pili
ya uchaguzi.
Hatua hiyo imezua wasiwasi mkubwa kwenye muungano wa Jubilee ambao
mgombea wake, Uhuru Kenyatta, amekuwa akiongoza kwa asilimia 54 huku
mpinzani wake Raila Odinga wa muungano wa CORD akiwa na asilimia 42
kufikia jana jioni.
No comments:
Post a Comment