Baraza
la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado
hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si
za kweli.
Hata
hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo
yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa
kutoa matokeo hayo mwezi Februari.
Ofisa
Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba
matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa
kijamii (Facebook).
Alifafanua
kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla
hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo
taarifa sahihi.
Aliwataka
wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa
tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa
kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu
zao za mkononi.
Chanzo Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment