Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.
Kutoka kushoto Katibu mpya Isidory Lyamuya, Mwenyekiti mpya Cosmas Wambura, Katibu aliyemaliza muda wake Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi.
*******
Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokwa Viongozi wa muda.
Katika
Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua
nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi.
Nafasi
ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya
Liberatus Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina
imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa
na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine zilizogombewa ni Wenyevitina
Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
Pia
kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi
Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa
ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga
Chama. Pia Katibu mya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama
wengine wote kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama
zaidi.
Baadhi ya wanachama wa Chadema walioshiriki zoezi la Uchaguzi la kupata Viongozi wapya wa Chadema Washington DC.
Mzee Emmanuel Muganda pamoja na Mkewe wakiwapa mawili matatu Uongozi mpya wa Chadema Washington DC. SOURCE: Swahili Villa Blog.
No comments:
Post a Comment