USIKU WA WEMA'S GLITTERED NITE ULIVYOFANA
Usiku
wa juzi watu kibao tulikutana kuzindua filamu ya superstar ya Wema
Sepetu.Kila kitu kilikuwapoa kuanzia mapambo,red carpet na burudani kwa
ujumla.
Kila
jambo huwa na mwanzo Mange Kimambi alitoa speech ya kuelezea jinsi gani
alimshawishi wema kushiriki miss Tanzania mwaka ule wa 2006.Wote
tunakumbuka ndio safari ya Wema Sepetu ilipoanzia.
Na mie nilikuwa miongoni mwa waalikwa gauni langu nililipata pale BEUTY POINTY kwa Aunty Faiza mpigie 0713 276486.
Tulikaa kuangalia japo kwa ufupi filamu ya superstar.MSIMAMO WANGU
Leo katika leo tena ndani ya movie leo Zamaradi aliniuliza nilionaje usiku ule?
Jibu langu la kwanza lilikuwa Ulikuwa mzuri lakini sikufurahi kwani nilitarajia mambo makuu 3.Uzinduzi wa tovuti,kampuni,na filamu.Badala yake ikawa ni filamu pekee why?Na hivyo ndivyo nilivyofahamishwa toka awali na nilikuwa na furaha juu ya hilo hata nilipokuwa nikiulizwa na watu wengi tu.Unakuta mtu anakuuliza hiyo wema sepetu ni nini nawajibu kwa mujibu wa nilichoelezwa.Badala yake sikuona hivyo viwili na mimi sikwenda pale katika shughuli kama mpambe bali Dina Marios wa leo tena ya clouds fm.
Pia zamaradi akaniuliza nimeionaje filamu?filamu ilikuwa inaonyeshwa vipande vipande hivyo sijui cha kusema maana sioni mwanzo ni upi wala ilipoishia.Ila ninachoweza kusema waliocheza wamecheza vizuri kwa Wema sina la kusema maana uwezo wake unajulikana pia nilimfurahia Barnaba.
Akaniuliza quality je?
Nikamjibu kwa quality sina uhakika maana tulikuwa tunaangalizia kwenye projector ambayo wakati mwingine hufanya picha ionekane vibaya tofauti na nitakavyoiona kwenye uhalisia.
Akaniuliza story vipi?
Nikamjibu kwa story ni yeye wema sepetu amecheza maisha yake binafsi kwa hiyo hapo sina cha kusema ila sijaona la kunishangaza sana.
Kubwa na mpongeza kwa guts za kuweza kufanya alichokifanya katika usiku ule ikiwemo kumleta Omotola Jolade ambae ni msanii mkubwa wa filamu Nigeria.Ukiwazungumzia wasanii wa kike Nigeria huwa anaanza Genevive Nnanji,Omotola Jolade,Ini Edo na Rita Domic.
KATIKA HAYO NILIYOYASEMA MTU ANASEMA NAUMUONEA WEMA WIVU?
Dina kuna kila dalili kuwa uko very much against Wema Sepetu, kama sio wivu basi Chuki tena uliopitiliza. Dina umeshindwa kusifia hata uthubutu aliouonyesha Wema na kumpa credit yake kwa umri wake na alichokifanya hata kama ingekuwa flop bado anahitaji pongezi za hali ya juu kwani ndio tukio la kwanza.nakubaliana na wewe kuwa huwezi kusifia kila kitu but...na ingawa ulijaribu kuwa movie critic lkn hukuenda into details kusema ni nini hukupenda. so were just bias. Briticism yako haikuwa constructive ni ukweli usipingika movie kwenye projector haitokuwa kwa ubora tunaoutaka but u still went ahead na kusema eti ulikuwa unamjenga how wakati everything to you was nothing. mimi kwa umri wangu 45 yrs age sina uthubutu alionao huyu binti na kama kulikuwa na makosa basi ni madogo madogo sana after all mistakes ni part ya uandamu na asie na makosa basi ana mapungufu. be positive na msifie mwanamke mwenzio. najua utaibania hii lkn I know uumbe utaupata. sikuchuki napenda tu kuwakilisha fikra kama nilivyokusikia. ni lazima tupendane jamani tushirikiane lets support each other adui wa mwanamke si mwanamke.
WIVU UTAKUUA KUJIFANYA UNA ROHO NZURI KUMBE HUNA LOLOTE, WATU WAMESHAKUGUNDUA, WIVU FANYA NA WEWE TUONE BASI
ANNOY HAPO JUU KWANI KUHUJUA KWAMBA DINA ANA WIVU, HATA ZILE PICHA ZA HARUSI YA YULE MTANGAZAJI MWENZAO WA ZNR HAKUZIONYESHA KIHIVYO MPAKA WATU WAKAMSEMA. WIVU ILE MBAYA ANAJI-PRETEND TU. HAPO KAKABWA ROHO, TAPIKA UPUMUE BI MKUBWA.
Sasa sijui wivu wangu uko wapi hapo kwani mimi muigizaji na chuki ya wapi tena?
Wema kila la heri nasubiri kuona filamu utakayofanya na Omotola Jolade najua unaweza na utafanya vizuri.Chanzo:http://www.dinamarios.blogspot.com/


1 comment:
hata mi naona una wivu sema hujijui maana hakuna hta kitu kimoja ulichosifia wakati watu wote wamependa na wanasifia kwenye ma blog, pia ulitaka ioneshwe movie yote mwanzo mwisho? mi nilikuwa nafatilia hii sikusikia kuhusu uzinduzi wa vingine labda we uliambiwa tofauti. ni kweli una wivu inaonesha dhahiri lakini hakuna ulichoharibu atasonga mbele unajitetea bure ila ndio hivyo ulishachemka na kutaka kuponda...pakinuka pamenuka hata ukipulizia perfume
Post a Comment