Wednesday, October 19, 2011

Benki Ya NBC Yazindua Huduma za Master Card


Mkuu wa masoko na mawasiliano wa benki ya NBC Mwinda Kiula Mfugale (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya master card ya benki ya NBC jijini Dar jana.katikati ni mkuu wa kitengo cha shughuli za kibenki wa benki hiyo William Kalaghe, na kulia ni  meneja wa card
 wa NBC Robert Mng"hanya. 
Meneja wa Card Ndg Robert Mngh"anya akitoa ufafanuzi juu ya matumizi ya Card hiyo mpya


NA DANIE SEMBERYA

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) moja ya benki kongwe sana nchini leo imezindua kadi ya mastercard ikiwa ni moja ya juhudi za makusuidi zinazofanywa na benki hiyo katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora mahali popte walipo nchini na duniani kote.

Kwa mjibu wa mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa benki ya NBC Bi. Mwinda Mfugale, mteja wa NBC sasa anaweza kupata huduma za kibenki katika mashine yoyote ya kutolea fedha (ATM) inayokubali mfumo wa MasterCard.

Mfugale ameongeza kuwa wateja wa benki ya NBC wanweza pia kufurahia na kuwa na amani kwani kwa kupitia kadi ya MasterCard unakuwa na uhakika kutoa fedha, kufanya manunuzi au kupitia huduma mbalimbali kwa kupitia mfumo huo mahali popote pale duniani.

“Ili kuhakikisha mteja wa NBC anafurahia na kuridhishwa na kadi yake mpya ya MasterCard, NBC tumefanya utafiti wa muda mrefu ilikuhakikisha tunakuja na kadi itakayokidhi mahitaji ya wateja wetu katika soko la fedha kitaifa na kimataifa,” amesema Bi. Mfugale.

Na kwa wateja wao wa zamani wanaotumia kadi zilizopo utaratibu umeshandaliwa ambapo mteja huyo akifika katika tawi lolote la benki ya NBC anapwe fomu ya kujaza na kasha kupewa kadi yake ya MasterCard kwa muda mfupi zaidi wakati wale wateja wapya watapaswa kufuata taratibu za kawaida za kibenki za NBC ilikufungua akaunti na kupewa kadi hiyo.

“Kuwa na kadi ya banki ni kitu kimoja , bali kuwa na uhakika wa kupata huduma bora isiyo na usumbufu kupitia kadi hiyo ni kitu kingine na ndio maana sisi katika NBC tukaona hatuna budi kuchukua muda wa kutosha kujipanga vizuri katika kila eneo ili mteja wetu aweze kufurahia huduma bora kupitia kadi yake ya mastercard ya benki iliyo karibu nawe kila mahali yaani benki ya NBC,’Bi. Mfugale ameongeza.

Naye mkuu wa kitengo cha shughuli za kibenki katika benki ya NBC Bw. William Kallaghe alisema “NBC imeamua kuzindua huduma hii kwa wakati huu baada ya kufanya uhakiki wa uslama wa hali ya juu ilikufikia viwango vya ubora vya kibenki na kimataifa,”. Na kuongeza kuwa huduma hii inapatikana kwa wateja wetu wapya baada ya kukamilisha utaratibu wa kufungua akaunti, na kwa wateja wetu wa zamani baada ya kujaza fomu za kubadili kadi zao za zamani watapata mpya,” alisemaKallaghe.

Kallaghe amewahakikishia wateja “Ningependa kuwahakikishia wateja wetu kuwa bei zetu za huduma ziko palepale na hamna mabadiliko yoyote kwa kipindi hiki,” Kallaghe alijisifu.

Kallaghe amewaomba wateja kujivunia huduma hii kwani kwani kadi hizi hupatikana papo kwa papo, tofauti na utaratibu wa zamani wa kusubiria kadi, kitu ambacho benki ya NBC imekuwa ya kwanza kuzindua.

NBC iliundwa Mwezi April, 2000 baada ya ubinafsishwaji na kuuzwa kwa benki ya ABSA ya Afrika Kusini inayomiliki Hisa asilimia 55 huku serikali ya Tanzania ikimiliki Hisa 30 na zinazobaki asilimia 15 zikimilikiwa na mashirika ya kifedha ya kimataifa.

NBC inamtandao wa matawi 54 nchini kote na mashine za kutolea fedha zaidi ya 250.

1 comment:

Anonymous said...

2gether we are saying thanks very much about your services(MasterCard) but on the other hand those improvement of technology are the among of the techniques of FREE MASONS to attract people in their culture(beliefs). Few people understand this issue....But am sorry!! Thanks 4 MasterCard,it is good,better & best 4 us.