Thursday, January 6, 2011

MAANDAMANO YA CHADEMA ARUSHA JANA


Viongozi wa CHADEMA katika maandamano leo kabla ya kutawanywa na polisi na wengine kutiwa mbaroni
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa mji wa Arusha wakiwa wameshika mabango katika maandamano hayo kabla ya wanausalama kuanza kuzuia maandanayo hayo.
Huyu Dogo pia nae alikuwepo katika maandamano hayo,ambapo naamini kabisa kwamba aliingia katika maandamano hayo kwa kufuata mkumbo tu.maana umri wake unaonekana ni mdogo sana.
Mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr. Willbroad Slaa.Mama Josephine Kamili akichuruzika damu mara baada ya kutokea kwa vurugu baina ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA dhidi ya Askari Polisi.Vurugu hizo zimezuka jana mchana huko mkoani Arusha mara baada ya kuzuiliwa kufanya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa na chama hicho.
Askari Polisi wakijaribu kulizuia gari moja lilikuwepo katika maandamano hayo.
Wanausalama wakimtuliza mmoja wa waandamanaji aliekuwepo katika maandamano hayo.
Wakazi wa maeneo ya jirani na zilipotokea vurugu hizo wakinawa maji usoni ili kupunguza makali ya sumu za mabomu ya machozi yaliyokuwa yakilipuliwa katika kutuliza ghasia hizo.
Mitaa ya Jijini Arusha ililindima milio ya Mabomu ya Machozi huku mitaa ikiwa imepoa kabisa.
Askari Polisi wakiwa wameenea kila kona kuhakikisha hali inakuwa shwari na hakuna mtu anaefanya maandamano hayo.Lakini kilichofuatias ni sekeseke kubwa.
Chanzo ni www.mtakwa mta.blogspot.com

3 comments:

Anonymous said...

Chadema 4 lyf.Simeo Henerico

Anonymous said...

Ndugu zangu nasikitika mno kwa yalliyotokea Arusha. mimi ni mfuasi wa CCM lakin kweli mmetutia aibu mno na kuanzia leo sikitaki chama chenu tena kwani mmeendelea kuwaifadhi mafisadi kama lowasa ni fisadi mkuu ndie anasababisha haya yote kwa kuwa alitaka kuuziwa maeneo mengi yakiwemo general tyre, jeshini azimio, na NHC.utadaiwa sana damu za watu, umeya mnangangania Arusha kuna nini kikwete? au ni haya mahotel yako ya kifahari uliyoyaweka katikati ya mbuga za wanyama ndo unalinda linda lakini usiuwe watu hivi. umekuwa mnyama kuliko mnyama mwenyewe kweli Mungu yupo. mmewaachafulia chadema mkutano wao wa nini angali walikuwa na amani yao ya kutosha na IGP mwema kama umeishindwa Tanzania nenda somalia shetani wewe. unasema watu wauliwe utakufa wewe Mungu yupo. acheni chadema wachukuwe madaraka kwani ni ya kwao kabisa mmechakachua ya uraisi hata ya umea na isitoshe inakuaje jimbo hilo unaligombania sana.sisi ufisadi wako wote kikwete tunaujua watoto wetu wanakufa na utapiamlo huku unaenda nje kila siku mmegawiana mashamba burka.naona unataka nchi yote iwe ya kwako na mwanao na lowasa mtakufa kwa laana za wananchi.sasa waachieni hawa viongozi wa chadema kwa aibu yenu siku hizi tumeshajua siasa msitufumbe macho hapa. lowasa lowasa lowasa mmeru uliyeama kabila shetani wewe acha nchi iende kama mungu alivyoipanga umeme umepandishwa kwa sababu ya kukulipa wewe tu.ulivyomnyama. nauli zinapanda kwa sababu yako gesi hivyohivyo.

Anonymous said...

Hawa ccm hadi wa2 waandamane na kupoteza raia ndio wakubali kuachia kiti cha umeya. Mwanza wametangaza meya kwa upande wa chadema bado arusha .Igola Gambaloya