KIF ENTERPRISES

KIF ENTERPRISES
MBEZI BEACH , DAR ES SALAAM

Tuesday, September 29, 2009

TO ALL TANZANIAN COMMUNITY LEADERS-UK
RE: INTERNATIONAL HIGH LEVEL CONFERENCE ON MWALIMU NYERERE TO BE HELD AT THE UNIVERSITY OF EDINBURGH, SCOTLAND 9TH NOVEMBER, 2009.

The Tanzania High Commission in London wishes to inform you about the above subject matter and a Nyerere commemorative publication we are promoting. The background to the matter is detailed below.
As you may already be aware, the University of Edinburgh in collaboration with this Mission and the Tanzanian community in Edinburgh are organizing an International High Level Conference focusing on the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, First President of the United Republic of Tanzania and a former student of the University of Edinburgh.
In honoring Mwalimu, The University has announced ‘The Julius Nyerere Masters Scholarship’, to a Tanzanian citizen for admission on a full time basis for a post graduate Master’s programme.

Two Tanzanians have been awarded the Mwalimu Nerere Scholarship for this academic year.
The Tanzania High Commission is promoting a Mwalimu Nyerere commemorative publication focusing on his influence and legacy as a leader. It is intended that the publication will feature a suitable reflection of Mwalimu’s influence across Africa and beyond, particularly the making of the Tanzanian nationhood and his role in the liberation of Africa as well as conflict resolution. We are approaching selected individuals across Africa and elsewhere to contribute articles for the publication.
The purpose of this note is therefore to request you to ask willing members of the Tanzanian Diaspora to provide articles. The articles should be of one to two pages.

The articles will be edited by the FIRST Magazine editors and there is no guarantee that all articles submitted will be published.

Although we have requested for specific topics from other people, we would like the Tanzanian Diaspora who wish to write to have more flexibility about the topics they would like to choose in relation to Nyerere’s legacy. This could be about his struggle for economic independence, new international economic order, the liberation of Southern Africa, his international stature and achievements and challenges.
The publication will be launched in London in October 2009, and as such we would appreciate to if articles are forwarded to us at least by the end of first week of October, 2009. Further, the High Commission would urge those Tanzanians who would be interested to travel to Edinburgh for the event, at their own expense, to register with the High Commission at the earliest.
The Tanzania High Commission wishes to thank you very much in anticipation of your contribution towards making this noble goal a reality.

TANZANIA HIGH COMMISSION LONDON.

KUMBE JUMA PONDAMALI SIYO MUAJIRIWA TFF

Juma Pondamali (kushoto) akizungumza na Mwalusako ambaye ni Katibu Mkuu wa timu ya Yanga.


Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) , Fredrick Mwakalebela , leo asubuhi akiwa kwenye ofisi za TFF zilizopo kwenye uwanja wa Karume , Ilala , jijini Dar es Salaam , amesema kwamba kocha wa makipa wa timu ya Taifa Stars , Juma Pondamali , siyo muajiriwa wa TFF isipokuwa anapigamzingo kwenye timu hiyo kwa kuwa kocha Mkuu wa Starts , Mbarazili , Maximo alimuhitaji .
Hata hivyo , Juma Pondamali ni kochawa makipa watimu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambapo TFF inatambua suala hilo.

Donors provide additional $23 million to UN for better development results


Hon. Mustafa Mkulo.Dar Es Salaam 29/09/2009 – Finland, Ireland, Norway, Spain, and the UK have made an additional $23 million available to the UN in Tanzania through the UN One Fund. These funds will be used, in cooperation with the government, for better development results in Tanzania.The One Fund is part of the Delivering as One pilot initiative in Tanzania which aims to improve development results delivered by the UN and its partners through increased programme coherence, harmonising business practices and communication amongst UN agencies, and increasingly working with government, through its systems.The Joint Steering Committee, on Thursday 24th September, approved the release of funds for the One UN Programme financial year 09/10. The Joint Steering Committee is co-chaired by the Permanent Secretary from the Ministry of Finance and Economic Affairs, the government’s lead ministry on UN reform, and the UN Resident Coordinator, the highest ranking UN official in the country.

This is the first year the UN has aligned its programming cycle to the government fiscal year - part of its effort to become a more effective development partner to the government.

The funds allocated will be spent on a number of the Joint Programmes which are part of the One Programme. These include:· Wealth creation employment and economic empowerment· Maternal and newborn mortality reduction· Support to national HIV/AIDs response·Capacity strengthening for development management·

Capacity building support to Zanzibar· Managing transition from humanitarian assistance to sustainable development in Northwestern Tanzania· Strengthening National Disaster preparedness·

Education·

Environment and Climate change.
This new allocation of funds is in addition to the $40 million the One Fund has contributed to development in Tanzania since its inception in 2008 through contributions from the above donors, as well as Canada, the Netherlands, and Sweden.The Joint Steering Committee is the core decision making body of the Government-UN and Development Partner governance structure. It oversees the implementation of the United Nations Delivering as One pilot in Tanzania.

Tanzania was among the eight countries in the world first selected to pilot of the Delivering as One reform initiative at country level.
Albania, Cape Verde, Mozambique, Pakistan, Rwanda, Uruguay and Viet Nam were the other seven. For more background information on UN Reform and coherence go to http://www.undg.org/.

When Zanzibar and Mainland veterans met...


A group photo of former national team players of Zanzibar (in red) and Tanzania Mainland before their recent friendly match in Zanzibar(picha na stori kwa hisani ya www.tff-tz.com).

KOCHA WA VIUNGOTAIFA STARS

Fredrick Mwakalebela , Katibu Mkuu waTFF.


Taarifa kwa vyombo vya habari.
29-09-2009


1. Kocha wa viungo wa Taifa Stars-MarceloGuerreiro hayko nchini kuanzia mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.
Kocha huyo alisafiri kwenda kwao Brazil baada ya kuomba likizo ya bila malipo kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo yanamkabili.Likizo hiyo ya bila malipo aliiomba kocha huyo niya miezi miwili na alikubaliwa na Katibu Mkuu wa TFF ambaye alisaini mkataba wa kazi wa kocha huyo.
Baada ya muda huo alioomba kocha huyo kumalizika, lakini matatizo yakawa hayajamalizika hivyo ilibidi kuomba tena aongezewe muda. TFF imeliangalia suala hilo na kumuongezea muda mwingine wa miezi miwili.
TFF imeamua hivyo kwa kuzingatia kuwa mwajiri pia anaowajibu wa kujali matatizoyanayomkabili mfanyakazi wake.
Matarajio ni kuwa baada ya muda huo ulioongezwa kumalizika matatizoya kifamilia yatakuwa yamemalizika ili kocha Marcelo aweze kurejea kazini .Iwapo baada ya muda huo matatizo yatakuwa hayajamalizika .TFF itaangalia la kufanya huko mbele .
MICHEZO YA TIMU YA TAIFA -TAIFA STARS.
Kulikuwepo na mipangoya kuwa na mchezo mmoja wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Oktoba 10 na Oktoba 14 ambao ulipangwa kuchezwa katika tarehe za mashindano za Fifa kwa vile mwezi Oktoba 2009 hakuna tarehe maalumu ya Fifa ya michezo ya kirafiki.
Jitihada za upata mchezo mmmoja wa kucheza hapa nyumbani hazikuzaa matunda.
Hata hivyo TFF imepata mialiko kadhaa ya kucheza michezoya kirafiki .Miongoni mwa moja ya mialikohiyoulitoka katika nchi ya Bahrain.
Mwalikohuoulieleza kuwa mchezo huoulipangwa kuchezwa huko Bahrain Jumapili Oktoba 4,2009.
Baada ya TFF kuangalia muda uliopo kuanzia tarehe ya kupata mwaliko, matayarisho ya Taifa Stars na safari , TFF imeamua kuwa mchhuo hauwezekani kufanyika katika muda uliopendekezwa.
Hata hivyoTFF imewaeleza Baharain kuwa tutaendelea kuwasiliana , na pale itakapopatikana fursa ya kucheza mchezowa kirafiki kati ya mataifa haya mawili basi hilolitaelekezwaz kwa kuzingatia ratiba na mipangilio yawakati huo.
Hivyo kwa sasa michezo itakayokuwa karibu kwa Taifa Stars ni ya Mataifa manne itakayodhaminiwa na kampuni ya Plus One hapo mwezi Novomba baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Frederick Mwakalebela.
KATIBU MKUU.

Monday, September 28, 2009

WANAFUNZI WA KIBASILA SEKONDARI WAGOMEA BARABARANI!


lEO asubuhi wanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila sambamba na shule ya msingi Kibasila kwa pamoja walikua na mgomo kutokana na eneo hilo la karibu na shule hizo kuwa na ajali za nyingi za mara kwa mara ambazo zimekuwa zinasababisha vifo kwa wanafunzi wa shule hizo.
Hivyo , kwa kushirikiana pamoja , wanafunzi wa shule hizo walijazana barabarani katika tukio hilo wanafunzi waliweza kuzuia baadhi ya magari yasipite katika eneo hilo likiwamo gari la jeshi lenye namba za usajili 2813 JW97 Defender na gari la polisi PT-0176.

maradona atema wachezaji saba

Maradona .Picha kwa hisani ya www.foxsports.com.


Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradona ambaye anajiandaa na mechi ya tarehe 10 mwezi ujao, amewatema wachezaji saba katika kikosi chake huku akimuita kwa mara ya kwanza mchezaji anayeitumikia klabu ya Real Madrid, Gonzalo Higuain ,ambaye anakipiga kwenye timu ya Real Madrid.

Kocha huyo, kwa mara nyingine amemwita tena kiungo Pablo Aimar jambo ambalo limewashtua mashabiki wa soka nchini hiyo kuwatema wachezaji saba ambao walikuwemo kwenye kikosi kilichobwagwa na Brazil na Paraguay katika kampeni za kusaka tiketi za kucheza kombe la dunia huko Afrika Kusini.


Argentina ambao ni mabingwa mara mbili wa Kombe la Dunia, hawajawahi kukosa kucheza fainali za Kombe la Dunia tangu mwaka 1970, ingawa kwa sasa wapo katika hatari ya kuzikosa fainali hizo huku wakiwa chini ya Maradona .

Kwenye taarifa waliotemwa ni Fernando Gago, Javier Zanetti, Jesus Datolo, Maxiliano Rodriguez, Lisandro Lopez, Pablo Carrizo na Nicolas Burdisso.

Timu hiyo ya Argentina itacheza na Peru Oktoba 10, mwaka huu nyumbani huku ikiwa imechapwa na Uruguay.
Kikosi kamili ni kitakuwa na makipa Sergio Romero, Mariano Andujar.

Walinzi: Pablo Zabaleta, Nicolas Pareja, Fabricio Coloccini, Gabriel Heinze, Emiliano Insua.

Viungo: Javier Mascherano, Jonas Gutierrez, Angel Di Maria, Pablo Aimar, Luis Gonzalez.

JOB OPPORTUNITY ....


Youth Action Volunteers (YAV) is a Non Governmental Organization registered in Tanzania in the year 2000. It has engaged in promoting equitable policy, service delivery, and governance in the health and HIV/AIDS sector in Tanzania.
The aim of our work is to achieve healthy and responsible young men and women with the ability to participate in their own development process, in order to realize Tanzania’s development vision 2025.
The primary target group is young men and women from the ages 10 to 24. YAV intends to enable greater social accountability within Tanzania by assessing district planning and resource allocation for the health sector and, expenditure and performance.
We are frequently seeking consultants who have experience in analytical work and the health sector.
The qualified candidate should have: At least Masters degree in Social Science or any relevant field Familiarity with the Tanzanian Social Accountability System Familiarity with the Health and Local Government Budgets and Health Budget Processes Familiarity with the context of Good Governance Ability to analyze and draw conclusions, policy recommendations, and implications for achieving an equitable health service delivery system in Tanzania. Interested consultants should send CV and cover letter to:
The Executive Director, Youth Action Volunteers, and P.O Box 12183, Dar es Salaam, Tanzania or by e-mail to mailto: href="mailto:info@yav.or.tz" target="_blank">info@yav.or.tz
jamaa.

MASHINDANO YA KIMATAIFA YA NETIBOLI KUANZA LEO DAR

MASHINDANO ya Kimataifa ya mchezo wa netiboli yanatarajiwa kuanzakufanyika leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo yanafunguliwa huku wenyeji Taifa Queens wakianza kupambana na Lesotho.
Taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha mchezo huo Tanzania (CHANETA), Anna Bayi, mechi nyingine ya leo ni kati ya Kenya na Malawi, iliyopangwa kupigwa katika uwanja huo.
Kuhusu kuwasili kwa timu zinazoshiriki, Bayi alifafanua kuwa hadi kufikia jana mchana timu sita tu ndizo zilikuwa zimewasili tayari kwa mashindano hayo yanayoanza leo hadi Oktoba 3.
Alitaja majina ya timu zilizowasili kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia ,Lesotho, Malawi, Namibia na wenyeji Tanzania .
Taarifa hiyo imesema kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo ya kimataifa atakuwa Mama Salma Kikwete.

WOSIA WA BABA WA TAIFA NA FISADI WA KIGIRIKI

Mwalimu Julius Nyerere (picha kwa hisani ya Nyerere Foundastion).


Wakati tukielekea katika siku za kumkumbuka Mwalimu Nyerere nimeona ni vema nikawakilisha kiaina jinsi Rais huyo wa Kwanza wa Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .Sasa hapa kuna Wosia wake ambao ni fimbo kwa mtu yoyote fisadi japokuwa ulimlenga tajiri mmoja wa Kigiriki enzi za utawala wa Rais Nyerere .
Lakini nimeanzia kati......
Nikaona lakini hata hivyo nitamfundisha tu.Nikamtia ndani.Nikatiwa msukosuko hapa na pale kwamba Mwalimu mwachie nikawaambia simuachi .
Mzee Kenyatta akaniletea ujumbe bwana huyu tunamfahamu ,mwachie nikamwambia simuachii hata kidogo .Simuachii .Siwezi kumuachia hana adabu anasema serikali yangu iko mfukoni mwake(kicheko).Simuachii hata kidogo.
Nikamwambia yule mama aliyetumwa na Kenyatta nikamwambia nenda kamwambie Mzee namheshimu sana lakini huyu mtu hatoki .Siku moja niko Msasani pale nikaambiwa anakuja ...kuna ujumbe Baba askofu kuja kukuona .
Anatoka wapi? Anatoka Kenya .Akaja.Baba Askofu wa Greek Orthodokxy ...Akaja Msasani kwangu pale .Akaniambia bwana ana ujumbe wangu . Nikamwambia njoo tuende katika kijumba.... pale Msasani ninakachumba kangu kadogo akanipa barua .
Naisoma barua inatoka kwa Baba Askofu Makarios . Mwalimu tafadhali umuachia huyo mtu .
Basi nikamwambia Askofu , tazama Baba Askofu, Huyu mtu mshenzi .Nadhani hata ninyi mnajua kwamba ni mshenzi . Sasa wamenifuata watu wengi , pamoja na kaka yangu kwa sababu kaka yangu alikuwa na marafiki zake Wagiriki wakanifuatafuata hapa Krismasi wakajazana tele hapa.Nikamwambia kaka yangu wacha...Wahuni hawa mimi sikubali .
Nikamwambia wamenifuata watu wengi ...nimekataa, pamoja na mkewe kanifuata nikamwambia siwezi kumuachia mumewo mtu wa hovyo.Sasa Baba wewe umekuja eh Baba Askofu.Barua yenyewe ya Baba Askofu Makarios .Sasa siwezi kukupeleka mikono mitupu.
Mpelekee habari Baba Askofu Makarios mwambie hivi : Mwalimu yuko tayari kumuachia .Lakini mumhamishe East Africa arudi Syprus akae hasionekane tena East Africa. Nikaletewa assurance (uthibitisho) kutoka kwa Baba Askofu nikamuheshimu nikamuachia .Sasa sijui kama aliwahi ...sikupata kumsikia tena.
Nwaambieni hadithi hiyo kwamba hatukuwa na utani utani juu ya mambo ya rushwa hatukuwa na utani na mtu.Rushwa ni jambo la hatari kabisa.

Baba wa Taifa alifariki dunia Oktoba 14, 1999, katika hospitali ya St. Thomas, jijini London, Uingereza.

Maandalizi ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Nyerere yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 14, katika kijiji cha Butiama mkoani Mara, alikozaliwa Mwalimu Nyerere mwaka 1922 .

Haya , sasa wasomaji wa blugi hii mnaweza kuwa na maoni na wosia huu.

Sunday, September 27, 2009

SHILINGI BILIONI 13 KUTUMIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Waziri wa serikali za mitaa na Tawala za mikoa (TAMISEMI) Mh. Selina Kombani amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa nchi nzima utagharimu jumla ya shilingi bilioni 13 fedha ambazo zimetengwa na serikali ili kugharamia mahitaji yote ya uchaguzi huo.
Waziri Kombani ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Wizarani hapo, amesema jumla ya vituo vya kupigia kura 60.359 vimetengwa katika maeneo mablimbali nchi nzima, katika utaratibu wa kupiga kura amesema kwa wapiga kura wa vijijini masanduku manne yatatumika katika kuwachagua wagombea kwa kila kituo na maeneo ya miji na majiji ni masanduku 3 yatatumika kuwachagua wagombea kwa kila kituo.
Kwa upande wa vijijini kutakuwa na masanduku ya kuwachagua mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kitongoji, wajumbe wa serikali ya kijiji mchanganyiko na wajumbe wa serikali ya kijiji kwa upande wa wanawake.
Kwa upande wa miji na majiji kutakuwa na sanduku la kuwachagua mwenyekiti wa serikli ya mtaa, wajumbe wa serikali mchanganyiko na wajumbe wa serikali kwa upande wa wanawake, waziri huyo ameongeza kuwa masanduku 180.000 yako tayari na yameshasambazwa katika mikoa ya kanda ya ziwa wakati kazi ya kutengeneza masanduku yaliyosalia inaendelea.
Mh. Selina Kombani amemalizia kwa kusema uandikiswaji wa wapiga kura utafanyika kwa muda wa wiki moja na baada ya kamaliza zoezi la kuandikisha wapiga kura litafuatia zoezi la kampeni kwa wagombea ambalo nalo litachukua wiki moja na kumalizia na uchaguzi hiyo Oktoba 25 mwaka huu nchini kote.

FIFA YATOA ONYO KALI KUHUSU TIKETI FEKI ZA 2010
Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA, mwishoni mwa wiki limetahadharisha mashabiki wa soka kutonunua tiketi za Fainali za Kombe la Dunia 2010 kupitia mitandao mingine zaidi ya ule wa Fifa kutokana na kuzuka mitandao ya kitapeli ambayo tayari imeanza kuuza tiketi feki .


Taarifa ya Fifa iliyosikika kupitia Shirika la Utangazaji la Uingereza , ilisema kuwa hatua hiyo inatokana na makampuni 20 ya Uingereza kufungiwa kufanya kazi ya kuuza tiketi za Kombe la Dunia kutokana na kutokamilisha taratibu zilizowekwa.


Fainali za Kombe la Dunia 2010 zimepangwa kufanyika Afrika Kusini kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 huku ikiwa ni mara ya kwanza fainali hizo kufanyika kwenye bara la Afrika.


Baada ya nchi ya Afrika Kusini kupata 'dili' la kuwa mwenyeji wa fainali hizo, kulizuka bahati nasibu kibao zinazowataka wadau wa mpira kununua tiketi kwa bei ya chee na kuingizwa katika droo kabla kuchezeshwa huku ikiwa si kweli. Hadi wakati huu zaidi ya tiketi 600,000 zimeripotiwa kuuzwa kabla ya fainali hizo za mwakani.

HIVI KANUMBA KWELI KIINGERZA HAKIPANDI ?

Steven Kanumba (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa bendi ya African Stars , Asha Baraka .
Kwa wiki kadhaa sasa vyombo kibao vya habari vimekuwa vikitoa habari inayomhusu Steven Kanumba kwa ishu yake ya huko Afrika Kusini kuwa eti alichemka baada ya kushindwa kuongea Kiingereza .
Hebu tujadili au kwa kupitia blogu hii Kanumba tuambie ukweli kwamba unapandisha mayai au hupandishi?

NI UTAMBULISHO WA SEPTEMBA 11

Benny Kinyaiya .


Huyu ni Ray kutoka kundi la Kaole , alikuwepo na kimsingi alikaa hadi mwisho wa utambulisho wa muvi hiyo . Hivyo ni msanii wa filamu aliyeshoo love ya hakika kwenye tukio hilo.

Jamaa anaitwa Mtanga , alikuwa chicha kinyama!! Licha ya kuwemo ndani ya nyumba , pia ameigiza kwenye muvi hiyo ambayo tayari ipo sokoni.


Huyu ni nyoa wa muziki wa Bongo Flava , Banana Zoro , yeye na bendi yake ya B Band ndiyo walitoa burudani na watu tukaruka kwanja kwenye kiwanja hicho kilichopo juu ya ghorofa la Millenium Tower.
Kipa wa timu ya Yanga , Obrien Krockivic (kushoto ) akiwa na demu huyu ....sasa sijui ni demu wake au ni jamaa yake?Lakini ni jamaa mcheshi sana hata kwa watu ambao hahuani nao!Pia kaigiza kwenye picha hiyo.Chidy Nassoro a.k.a Mzee wa Mbele abaye ni promota maarufu wa mchezo wa ngumi hapa Tanzania na pia ni muigizaji wa filamu , jana naye alikuwemo ndani ya mjengo na nilipiga naye stori mbili tatu hivi kiutuuzima.

Baadhi ya watu waliotimba jana Millenium kucheki mambo.


Mtangazaji wa Star TV , Sauda Mwilima alizama ndani ya Mzalendo Pub na kwa hakika ni kati ya demu aliyekuwa kapiga pamba hasa kiasi kwamba nilipomuona tu nikajua leo kuna makubwa ndani ya mjengo huo!

JB ama mimi huwa napenda kumuita kubwa lao! Alikuwemo kwenye mjengo lakini aliniambia kuwa anappenda nimpige picha akiwa hivyo!!!
Wakati utambulisho wa filamu hiyo ukiendelea , Frederick Mwakalebela alisema ndani ya filamu hiyo pia yumo kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo, aliyeigiza kama daktari.
Mbali na Kocha huyo pia Mwakalebela ameigiza pamoja na wachezaji kipa Juma Kaseja na Mussa Hassan Mgosi wa Simba pamoja na kipa wa Yanga Obrien Krockivic.
Aidha, wamo waigizaji Charles Magali, Yusuph Mlela, Flora Mvungi, Jacqueline Wolper, , Benn Kinyaiya, Kulwa Kikumba 'Dude' na wengine kibao.Saturday, September 26, 2009

MASHAIRI YA WIMBO " NYOTA YANGU' TID

Tid ni wa mwisho kulia .Kiitikio
Jua kwamba wewe ndio wangu baridi ya roho 'seisha na hamu sura yako dawa kwangu raha za pungu' kando zangu mahaba yako ndio tiba yangu nyota yako yang'ara yangu


Ubeti wa kwanzaHebu tathmini kisha nipe jibu'vi kwanini hutaki kunijibumitihani yote nimeshindanadhani ni wakatipenzi letu sisi liwe waziroho yangu inauma (maumivu sasa basisasa basiiiii

Ni kwa thabiti nielewepesa sio mapenzi...pesa sio mapenzi...kwa utenzi huunielewe babynakuhitaji mpenziwewe nd'o faraja yanguWewe nd'o faraja yangufaraja yanguyou are my baby...Jua kwamba wewe ndio wangu (oohhh...)

baridi ya roho 'seisha na hamu (faraja yangu)sura yako (yako) dawa kwangu (kwangu mimi) raha za pungu' kando zangu (nd'o zangu)mahaba yako ndio tiba yangu (tiba yangu ti..)

nyota yako (ehh..)

yang'ara yangu (Kwangu mimi)

Kama tamaduni zetu ni mojatwende nyumbani ukamsabahi mama tupate baraka za wazazina uwajue ndugu zangudini zetu isiwe kama hojapingamizi sintozingojaniko tayari kukuvisha peteuwe wangu... kwa utenzi huuniamini (niamini)

nielewe (nielewe)

coz you're my baby (yeah yeah)

you're...you're my ladynjoo nyumbani njoo nyumbaniyou're my lady njoo nyumbaniunipe burudani yeah uliniaminiyou're my lady njoo nyumbaniunipe burudaniUnione kama mimi yeah yeah ya'Jua kwamba wewe ndio wangu(nd'o wangu) baridi ya roho 'seisha na hamu (faraja yangu)

sura yako (yako) dawa kwangu (kwangu mimi)raha za kungu kando zangu (nd'o zangu) mahaba yako ndio tiba yangu (tiba yangu ti..)nyota yako (ehh..) yang'ara yangu (Kwangu mimi)Jua kwamba wewe ndio wangu (nd'o wangu)

baridi ya roho 'seisha na hamu (faraja yangu)sura yako (yako) dawa kwangu (kwangu mimi) raha za kungu kando zangu (nd'o zangu)mahaba yako ndio tiba yangu (tiba yangu ti..) nyota yako (ehh..) yang'ara yangu (Kwangu mimi)

HAPA NI SCHENGEN NIGHT CLUB-KINOLiva Hassan Sultan ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Diamond Sound na pia ndiye Mtendaji Mkuu wa Schengen , hapa alikuwa pozi kwa ajili ya picha hii , baadaye alijiunga na jamaa zake hapo chini na kuanza kunywa kwa sana tu.
Kwenye mazungumzo yetu alidokeza kuwa yupo mbioni kuingia studio kurekodi traki yake nnje ya bendi , hiyo inaitwa ' Long Story ' hata hivyo bado hafahamu ni studio ipi itafanya kazi ya kurekodi traki hiyo.
Watu wakiamua kufanya mambo wanafanya!!!


DIOF AIMBA NA AKUDO IMPACT-MANGO GARDEN

Rapa namba moja wa bendi ya Akudo Impact , Toto The Bingwa (mwenye Maiki) akirapu huku akipewa tano na mashabiki bendi hiyo, hii ni jana usiku pale Mango Garden , Kinondoni , jijini Dar es Salaam.Rapa wa bendi ya African Stars , Msafriri Diof akichana mistari huku akiwa na mpenzi wa muziki.


Nyota wa muziki wa Bongo Flava , Dully Sykes(mwenye tisheti ny
ekundu) naye uzalendo ulimshinda akaamua kushika maiki na kuanza kuimba huku akijishebedua kama kawaida yake!Hata hivyo alipafoumu kichizi na watu wote walimpa tano.

Huyu ni mcheza shoo wa Akudo Impact.Yeye bize na kiouno viono.
TOTO AFRICA KUKIPIGA NA AFRICAN LYON JIONI HII

Katibu Msaidizi wa timu ya Toto African , Heri Kange.
LEO Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara , inaendelea tena kwenye uwanja wa Uhuru ‘ Shamba la Bibi ‘ ambapotimu ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam itashuka dimbani kuikabili Toto Afrika ama ‘ Wanakishamapanda ‘ ya huko jijini Mwanza ambazo zote zinasua sua kujinasua kutoka mkiani mwa hiyo.
Mechi ya leo inatarajiwa kuwa kali kwani timu hizo zinakutaka zikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mechi zao za mwisho ambapo Lyon ilifungwa 1-0, wakati Toto ilikutana na kipigo kama hicho kutoka kwa Manyema Rangers,mechi zote zilifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

BATA ZINAENDELEA !


Hafsa Kazinja.Jana saa kumi na mbili jioni Hafsa Kazinja alinidokeza kwamba amekamilisha kuchukua picha za matukio za video yake inayoitwa Baleke ambayo kaiimba kwa kumshirikisha mwanadada Lady Mariam wa Uganda .Traki hiyo imerekodiwa huko huko nchini Uganda na imeimbwa kwa Kinyankore .Selles Mapunda (kushoto ) halafu anafuata Hafsa Kazinja kisha Richard ambaye amewahi kuwa mshindi wa Big Brother Africa (2007) . Hapa Riki Hotel maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo niliwakuta wakizungumza juu ya komedi mpya ambayo ipo mbioni kuruka hewani kwenye vituo vya runinga.

Friday, September 25, 2009

NASIKIA TUNDAMAN NA SPARK KILA MTU KACHUKUA HAMSINI ZAKE !

Spark akichonga kwenye simu .Mwenye tisheti ni Spark akiwa na Tunaman . Hapa walikuwa bado washikaji , ilikuwa ni siku fulani hivi nilipokutana nao nnje ya jengo la Kitega Uchumi jijini Dar es Salaam .

Taarifa zilizopo kwenye vijiwe hasa hasa vya muziki wa Bongo Flava ni kwamba , ule ushikaji kati ya Tundaman na Spark umefika kikomo na sasa kila mmoja anafanya mambo kivyake tofauti na ilivyokuwa hapo awali . Mdudu gani tena kaingia?

WASANII HAMJUI OFISI ZA COSOTA ZILIPO?

Ndani ya jengo hili kuna ofisi za COSOTA.
Hizi ni picha zilizopo kwenye kava la filamu mpya inayoitwa New Page.


LEO nimekutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki za Wasanii (COSOTA ), Yustus Mkinga ambapo amefafanua kuwa tangu COSOTA imeanzishwa imekuwa ikipambana na maharamia wa kazi za wasanii pamoja na kupigania (mrabaha), na malipo ya kazi za wasanii kutoka katika vituo mbalimbali vya redio, runinga na kwenye kumbi mbalimbali za starehe hapa nchini.
Isitoshe alizidi kubainisha kwamba mwezi uliopita wamegawa malipo ya haki za wasanii kutoka katika vituo hivyo kiasi cha sh milioni 80 na wasanii wapatao 1,080 walipata mgawo kama inavyopasa.

"Mara kwa mara huwa nasikia tu kwenye vyombo vya habari kuwa kuna wasanii wanalalamika kwamba ofisi yetu haifanyi kazi ipasavyo, lakini nikiangalia jina au majina ya wasanii hao wanaolalamika natambua mara moja kwamba hawajawahi kuja ofisini kujisajili ! Sasa nabaki nashangaa tu na kujiuliza maswali kibao kwamba wanawezaje kulalamika bila hata ya kuja kwanza kujisajili kwetu halafu hayo mambo mengine yakafuata?"Alisema Mkinga nilipokutana naye leo juu kwa kwa juu huko mitaani.


OFISI ZA COSOTA ZIPO KWENYE JENGO LA KITEGA UCHUMI JIJINI DAR ES SALAAM.

Thursday, September 24, 2009

ZAWADI YA SEPT NA SHINDANO LA UNIQ MODO
100.000/= ZAWADI YA MWEZI SEPTEMBA!!!!
Tumemfikia Septemba modo namba 7!!! Naambiwa picha tele zinakuja.
KUMBUKA, KUSHINDA LAKI MOJA KWA SEHEMU KUBWA INATOKANA NA MODO KULETA PICHA YAKE MWENYEWE KWENYE BLOG AMA AKITUMA UJUMBE KWAMBA YUPO TAYARI KUPIGA PICHA JUMAMOSI AMA JUMAPILI MCHANA.
KAMA UNA PICHA ZAKO MWENYEWE, TUMA kupitia tgliundi@gmail.com

Siku ambapo mshindi wetu atapokea zawadi yake ya LAKI MOJA taslimu, ni siku ambapo UMODO itatangaza tamasha na shindano lake maalumu na la aina yake nchini ambapo modo mkali atashinda FEDHA TASLIMU MILIONI MOJA!!

ITAKUWAJE?
1. Octoba 5 tutakaribisha wasichana kutoka kila kona ya Dar kwa mara hii ya kwanza, ambao wanajiamini wanaweza kuwa modo ama ambao tayari ni modo kujiandikisha kushiriki kwenye shindano la Uniq Modo.
2. Shindano la Uniq Modo litakuwa na hatua mbili kuu.
3. HATUA YA KWANZA: Usaili wa wasichana na kisha kuchaguliwa kwa wasichana 12 kwa njia ya mchujo maalumu na majaji. WASICHANA WOTE 12 watakaopita watapata LAKI MOJA kila mmoja!
4. HATUA YA PILI: Wasichana 12 kuingia rasmi kwenye shindano la mwezi mzima.
5. Shindano litafanyika mamodo wakiwa kambini na wakati mwingine wakiwa majumbani. Popote pale watakapokuwa, na kwa ratiba maalumu ya shindano, camera zetuzitawafuata. Vipindi vya mfululizo wa matukio vitatoka kila siku ( ama kwa ratiba maalumu) kwenye Tv. Magazeti wadhamini watatoa picha na maelezo ya shindano.
6. Shindano litaisha na tamasha kubwa la maonyesho ya mavazi na ubunifu wa mamodo wenyewe, wabunifu alikwa maarufu na chipukizi!
7. Modo mshindi ataondoka na MILIONI MOJA. Wengine watapata zawadi za kuvutia za fedha na zawadi za wadhamini wetu.

Vigezo vya kuchaguliwa vitatajwa muda ukifika, lakini ningependa wasichana wote, wembamba, wafupi, wanene, weusi, weupe mjisikie poa maana tunatafsiri upya UMODO! Swala tu ni uzuri wa ngozi, uhalisi.

JE, KATIKA MWEZI MZIMA, MODO ANASHINDANA VIPI? Hapo ndipo patamu, kwa kweli hatuwezi kusema sasa. Muda ukifika, mtajua, lakini nawaahidi kwamba ni ubunifu ambao hadi nchi za nje wataiga!! Itakuwa ni burudani, elimu na msisimko mkubwa kwa washiriki na watazamaji ama wafuatiliaji!!

Niliahidi kugeuza mchezo huu, NA SASA ITAKUWA KWELI. Kama unasoma haya, mfahamishe mwenzako anayependa mambo ya umodo, ubunifu na urembo ajiandae.

Wadau wa umodo ambao mna maduka ya mavazi na urembo, tuwasiliane ili mshiriki katika tamasha hilo la umodo litakaloitwa UNIQ MODO! Tunakaribisha hadi wauzaji wa mitumba bora katika maeneo ya Dar es salaam. Pia nakaribisha madesigner na washonaji chipukizi tu kwa sasa.


TAFADHALI TUWASILIANE MAPEMA!
Tuma ujumbe hivi sasa kama ungependa kushiriki:
0655 888 799!!

MABOMU YA MBAGALA YALIPUKA TENA!!!

Habari za uhakika zilizoifikia blob hii leo asubuhi zinaeleza kuwa Watoto wawili wamekufa kwa bomu maeneo ya Mbagala Kizuiani karibu na kambi ya Jeshi, wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Chanzo chetu kimebainisha kwamba watoto waliofariki ni Regina Chawala (6) na Rajab Said (6) ambapo katika mlipuko huo , kulikukuwa na majeruhi wanne ambao hata hivyo bado hawajatambulika majina yao.
Mwanzo wa Mlipuko hiyo imetajwa kuwa ni mabaki ya mabomu kufuatia mlipuko kwenye kambi ya Jeshi iliyopo karibu na makazi ya watu wa maeneo hayo .

UMEWAHI KUKAMATWA NA POLISI BARABARANI?


Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !
Bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani kutakuwa na vurugu katikabarabara zetu.
Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara – iwapo kila mmojaatazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao,isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.

Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani.

Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako – lakini kumbukakwamba ni mwongozo tu.

Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako – kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani – piaanaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).

Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari – anaweza kukataa fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupelekaleseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.Ili kuepukamatatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).
Hati ya usajili: Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu vidogokama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).
Leseni ya barabarani, na bima ya gari: Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani nakibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).
Kunyang’anywa: Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseniisipokuwa kwa mujibu wa sheria.
Mikanda ya kiti ya usalama: Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) – unatendakosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.
Kuendesha baada ya kunywa pombe:Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi chapombekwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatiaya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).
Kutumia simu ya mkononi wakatiunaendesha: ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).
Mwendo kasi: Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisianaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unawezakupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73(2)).
Kustahili kuwepo barabarani: Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.
KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA: Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwaofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishikwa Ofisa Msimamizi Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu –usitoe rushwa na usipokeerushwa.
Said A. Mwema (Inspekta Jenerali wa Polisi) .

TFF YAITUPA RUFAA YA YANGA

Zamunda (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Yanga Iman Madega jana kwenye ofisi za TFF, Ilala , jijini Dar es Salaam.

Kamatii ya Nidhamu ya Shirikisho la soka nchini (TFF) jana iliitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Yanga ikipinga usajili wa mchezaji, Uhuru Suleiman wa timu ya Simba.
Rufaa hiyo ya Yanga ilikuwa inapinga mchezaji huyo aliyeichezea Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro msimu uliopita kwamba amesajiliwa nje ya muda uliowekwa na TFF.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jana kutoka katika kikao cha kamati ya nidhamu , rufaa hiyo imetupiliwa mbali na Simba haitanyang'anywa pointi kama ambavyo Yanga ilivyokuwa inadai.
Hivyo, matokeo ya uwanjani ya mechi zote ambazo mchezaji huyo ameichezea timu yake ya Simba yatabaki kama yalivyokuwa na hivyo kutokuwa na mabadiliko ya aina yoyote.

RESTITUTA MAIGE AIBUKA NA KITITA DAR ES SALAAM


Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Selcom Gaming Limited , Julio Batalia (kushoto) akiwa na Meneja Masoko wake Juma Mgori.
Kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Selcom Gaming Limited , Juma Mgori akifuatiwa na Maggid Bakari kutoka Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa wakimkabidhi amfano wa hundi ya thamani ya shilingi Mil. 5 , mshindi wa tano wa bahati nasibu hiyo, Restituta Maige ambaye anaishi maeneo ya Kijitonyama , Dar es Salaam , hii ilikuwa leo saa tano asubuhi kwenye ofisi za Selcom , mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam .

MICHANGO YA FEDHA KWA NJIA YA SIMU SIMBA ,YANGA .

lucas kisasa .


ILE Michango ya fedha kwa njia ya simu kwa timu ya Simba na Yanga bado ni kitendawili
licha ya Kampuni ya Push Mobile Media Ltd kusema iko katika mchakato wa kuzilipa klabu za Simba na Yanga fedha zilizopatikana kutokana na huduma za ujumbe mfupi wa 'Fan Club' unaotoa taarifa mbalimbali za klabu .
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa pamoja na mikataba kuingiwa kati ya kampuni hiyo na timu hizo, lakini bado kuna utata fulani kwa malipo kamili kwa fedha zilizopatikana kwenye mpango huo mzima.
Kwenye mpango huo , kila mwanachama au shabiki wa Simba au Yanga amekuwa wakikatwa sh150 kwa kila ujumbe anaopata.
Taarifa za awali zilisema kuwa, kutokana na mpango huo, klabu ya Simba imeingiza wanachama na mashabiki 30,000 wakati Yanga ni 14,000 waliojisajili.
Kwa mpango uliowekwa, timu hizo zinapata sh50 kwa 'meseji' moja kati ya sh150 na sh 50 nyingine inakwenda kampuni ya simu ambayo mtandao wake umetumika na nyingine inaingia Push.
Mitandao ya simu ambayo imekuwa inatumika ni Zain , Vodacom, Tigo, TTCL, Sasatel ambapo huratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA).

Yanga inatarajia kuvuna sh. 700,000 endapo meseji zote 14,000 ziliwafikia mashabiki na wanachama wake waliojisajili katika huduma hiyo, lakini fedha hizo zitakuwa zaidi endapo wanachama na mashabiki hao 14,000 watatumiwa ujumbe mara nyingi .
Kwa upande wa Simba ambayo imepata wanachama na mashabiki 30,000 na kutokana na makato hayo kwa mtu mmoja na sms moja, Simba inaingiza shilingi milioni1.5 na pia itakuwa zaidi endapo watu hao watatumiwa ujumbe huo zaidi ya mara moja.
Hata hivyo, Afisa Mwandamizi wa Kampuni ya Push Mobile, Rahim Kangezi alisema kuwa mabadiliko ya uongozi ya hivi karibuni ya timu hizo ndiyo imekuwa kikwazo cha timu hizo kupata mkwanja huo hizo.
Afisa huyo alizidi kufafanua kuwa kwa wakati huu wapo mbio mbio katika mpango wa kuzilipa timu hizo , ambapo malipo yake yanatatokana na idadi ya wanachama waliojisajili kwa ajili ya timu zao hapo siku za nyuma.
Alisema kuwa walifanya kikao na watendaji wapya wa klabu hizo na kukubaliana njia yakupata malipo yao ndani ya wiki moja.
Katibu mkuu wa zamani wa Yanga, Lucas Kisasa , amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo na lolote linalo husu Yanga kwa kuwa hayuko ndani ya klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega ambaye nilikutana naye jana kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), alikiri kwamba kuna asilimia fulani ya fedha wanaipata kutoka kampuni hiyo lakini hakutaka kuendelea kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi.
Katibu Mkuu wa Simba, Mwina Kaduguda alikataa kuzungumzia suala hilo na kuelekeza aulizwe Afisa habari wa Simba , Clifford Ndimbo.
Hata hivyo, jana na leo sikuweza kumpata Ndimbo .

SAID HAMIS KUTOKA SUMBAWANGA AIBUKA NA PIKIPIKI

Hapa Said anaiwasha Pikipiki yake kwa mbwembwe f 'lani hivi !

Said Hamis ambaye ni mkazi wa Sumbawanga , ameibnuka mshindi wa bahati nasibu maarufu ambayo huwa inaendeshwa na redio CLOUDS FM kwa kushirikiana na STEPS ENTERTAINMENT kupitia kipindi cha MOVIE LEO ambacho uendeshwa ndani ya kipindi cha Leo Tena.Leo saa nane mchana mshindi huyo amekabidhiwa zawadi ya pikipiki yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu (750.000) ambayo imetolewa na kampuni ya KISHEN ENTERPRISES ya jijini Dar es Salaam.
“Draw hii ilianza rasmi siku ya tarehe tano January mwaka huu ambapo mara ya mwisho ilichezeshwa miezi miwili iliyopita, hii ni mara ya saba kwa draw hiyo kuchezeshwa ambapo mshindi wa mwezi ametokea Sumbawanga , Lukwa.”
Alisema Zamaradi H.
Mketema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo saa tano asubuhi kwenye ofisi za Steps Entertaiment zilizopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Aidha , Mratibu huyo wa shindano hilo la bahati nasibu inayochezwa kila mwezi, aliendelea kufafanua kwamba filamu ambazo zimeshindanishwa kwa mwezi Juni ni Full Moon, It's Too Late na My Book ambapo kuponi za ushiriki wa bahati nasibu hiyo zinapatikana nyuma ya nakara halisi ya filamu zilizoorozeshwa hapo juu.
“Mbali ya ununuzi wa filamu filamu hizo , pia draw hiyo inahusisha filamu zote zinazo sambazwa na Steps Entertainment “.
Aliongeza kusema Zamaradi Mketema.
Lengo kubwa la draw hiyo ni kuwaamsha Watanzania ili waweze kununua kazi zilizo halisi kwa maana ya original kopi ambapo nia ni kupiga vita uharamia wa kazi za filamu unaofanywa kupitia ununuzi wa kazi zilizo feki ambazo hutengenezwa na Watanzania wachache wanaorudisha nyuma Industry ya filamu hapa nchini.
NUNUA HALISI UWE HALISI.Kushoto ni mratibu wa bahati nasibu ya shindano hilo , Zamaradi Mketema akifuatiwa na mshindi wa mwezi huu , Said Hamisi wakati wa kukabidhiwa zawadi yake ya Pikipiki kwenye ofisi za Steps , leo mchana .
BIG BROTHER AFRICA .....

PALOMA - ZAMBIA .BIG BROTHER REVOLUTION saw alliances wobble, new rifts open, romance bloom and tensions rise – with a bit of dance thrown in!After the morning's exercise routine, Liz pulled Nkenna aside to find out where she stands in the house.

When Nkenna had no answer, Liz told her that she was concerned that some of the women have forgotten their "Woman Power Pact" and are falling for the men. Liz tells Nkenna: "We have to take them out, one by one - otherwise we won't survive.

"During a whispered strategy session, Kevin told Paloma that with her help, they could "take out" the ‘Smokers’. Paloma voiced her concerns about the divisions growing between the ladies. She reckons that the Twins and the rest of the Smokers believe that she is masterminding their nomination, which has put her under threat.

Kevin still thinks that the Smokers believe that Erastus and Edward's nominations were part of Big Brother's trickery and not the work of an alliance.Kevin tried to convince Paloma that his alliance, consisting of Itai, Quinn, Jeremy, Leonel and Kaone, is the way to go. Paloma told him that she is weary of the three musketeers: Liz, Jennifer and Kristal, and that she is still testing the waters with them.

Wednesday, September 23, 2009

KOCHA WA AZAM AJIGAMBA
Kocha Mkuu wa timu ya Azam FC (Tamtam), Mbrazil , Itamar Amourin , leo saa tisa mchana nilikutana naye kwenye ofis za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ,Ilala ,Dar es Salaam , ambapo alijigamba kwamba timu yake inauwezo mkubwa wa kuibuka bingwa wa Ligi ya Tanzania Bara mwaka huu.

Kwa sasa Azam inashikilia nafasi ya huku ikiwa na pointi saba katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Simba yenye pointi 15 huku ikiwa haijapoteza hata mechi moja.


DJ MAKEI YUPO NANANIVILE?


Ilikuwa ni siku ya Sikuu ya Idd pale Mzalendo Pub , pichan ni Dj Makei (kushoto ) akiwa na mwanadada Kemmy Mtahaba .
Licha ya kuwabamba siku hiyo , pia siku ya pili yake yaani Iddi Pili niliwabamba tena kwenye kiwanja hicho hicho wakiendeleza libeneke! Hadi sasa bado sijaelewa hawa jamaa wanaurafiki upi?

HAPA NI COCO BEACH SIKU YA IDD MOSI

Wakazi mbalimbali wa jijini Dar es Salaam wakiwa wamekusanyika maeneo ya ufukwe wa Coco Beach kusheherekea Sikukuu ya Idd El Fitri .
Kulikuwa na nyomi si la kitoto huku watoto wakipoteana kwa sana tu. Hata hivyo hakuna taarifa zozote zilizopatikana kwamba kuna mtoto au watoto waliopotea .

Saturday, September 19, 2009

Alliance Française has the pleasure to invite you to the official opening of a Paintings exhibition


Two great Tanzanian painters from Zanzibar:Soud Seif and Hamza M. Ausiy
Soud Seif started his career as painter in 1998. His artwork deals widely with daily life he paints light and tone work. He participated in art exhibition in USA, Mauritius and Tanzania (Zanzibar and Dar es Salaam).

Hamza M. Ausiy was born in Zanzibar in 1966. In 2003 he was recommended in the East Africa Residency in Nairobi, where he had enough time to create his style and technique.

His paintings are monochrome, half breeding of impression and abstract using palette knife on canvas. Most of his works were influenced by the environment, history and culture of Zanzibar. He exhibited in Zanzibar, Dar es Salaam, Nairobi, South Africa and America.
Now he works as full time artist in ZAYAA GALLERY studio in Zanzibar.Alliance Française Exhibition Hall
Official opening on Thursday 24 September, 6.30pm.Open 25 Sept - Saturday 10 Oct., Mond. to Sat. 10am – 7pm
Entrace Free! Exposed works will be sold for the sole benefit of the artists.More info: ALLIANCE FRANÇAISE Your French Language and Cultural Centre in Dar es Salaam French courses, Resource centre, Films, Exhibitions, Concerts.
Phone: 21 31 406 / 0755 481 374 cultural@afdar.com www.ambafrance-tz.org
Ali Hassan Mwinyi Road(car park behind Las Vegas Casino)
Office opening hours: Mon-Fri: 9am-1pm / 2pm-6pm /Sat: 10am-5.30pm

TIMES FM KUFANYA MAMBO SLIPWAY

Times FM and Msasani Slipway LTD , brings you Eid Day from 15 hours up to 0:00 hours .Come with your family and friends to get a good entertainment for childrens and music from Times Fm Djds.

WISHES YOU ALL EID MUBARAK.....


King Kif Productions wishes you all Eid Mubarak . May the guidence and blessings of Allah be with you and your family......

SIMBA YAIFUNGA MANYEMA

Timu ya Simba ama Wekundu wa Msimbazi ya jijini Dar es Salaam , jioni hii imefanikiwa kuifunga timu ya Manyema kwa goli 2-0 katika Ligi Kuu ya Vodacom mechi ambayo imechezwa katika uwanja wa Uhuru ama ' Shamba la Bibi ' jijini Dar es Salaam .
Goli la kwanza la Simba limefungwa na Hilaly Echese kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha kwanza ambapo bao la pili limefungwa na Danny Mrwanda kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Manyema ama ' Mkuki wa Sumu ' kuunawa mpira kwenye eneo la hatari . Kwa matokeo hayo sasa Simba imefikisha pointi 15 na inaendelea kushika uskani wa ligi hiyo inayoshindaniwa na timu kumi na mbili .