UHURU PEAK KINONDONI

kif mwenyewe!

kifltd

KING

BLOGU HII INAKULETEA HABARI MBALIMBALI ZA JAMII, SIASA, MUZIKI, MITINDO NA MICHEZO.


Sunday, March 4, 2012

Mhe Jakaya Kikwete Ziarani Moshi




  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi jioni hii.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha   walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hiitayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
PICHA NA IKULU 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi jioni ya leo, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.
Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010

SIMBA YAIFUNGA TIMU YA KIYOVU YA RWANDA 2-1


Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi kulia akijaribi kumtoka mchezaji wa timu ya Kiyovu ya Rwanda wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho katika ya timu hiyo na Kiyovu ya Rwanda unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Simba imefanikiwa kuiondosha Kiyovu ya Rwanda magoli 2-1, magoli ya Simba yamepatikana katika kipindi cha kwanza na yamefungwa na mshambuliaji Felix Sunzu akipokea pasi nzuri, kazi iliyofanywa na mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba. Timu ya Kiyovu imefanikiwa kupata goli lake la kwanza katika kipindi cha pili cha mchezo huo, hata, Simba imefanikiwa kusonga mbele katika mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,
Wachezaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wakishangili mara baada ya mchezaji Felix Sunzu kufunga goli la pili kati ya magoli mawili aliyofunga
Timu zikiingia uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo huo jioni hii.
Mashabiki wa Simba wakishangilia kwelikweli wakati timu hizo zikicheza.
Kulikuwa n a kila shamrashamra kwa mashabiki wa Simba kama unavyowaona katika picha.
Hii inaashiria kwamba kama matokeo yatakuwa hivihivi mana yake ni kwamba Simba itaendelea kukwea Mwewe yaani Ndege kwa ajili ya kushiriki raundi ya pili ya michuano hiyo.
Chanzo Full shangwe 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste la Welfare Ministry of Africa, Stanley Mnai akivikwa pete ya ndoa na Bibi Harusi, Gloria Kaserwa


Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste la Welfare Ministry of Africa, Stanley Mnai akivikwa pete ya ndoa na Bibi Harusi, Gloria Kaserwa katika kanisa hilo lililopo eneo la Vetenari, Temeke jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Katikati ni Askofu Msaidizi, Upendo Mnai, ambaye ni mama mzazi wa bwana harusi. (Na Mpigapicha Maalumu).

.....
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kipentekoste la Welfare Ministry of Africa, Stanley Mnai amefungishwa ndoa takatifu na mama yake mzazi ambaye pia ni Askofu Msaidizi wake, katika misa ya 40 Kibaha ndoa iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo lililopo eneo la Vetenari, Temeke jijini Dar es Salaam.

Kanisa hilo lililoanza rasmi mwaka 2009 na kuvuta waumini wengi, lina viongozi wawili tu wenye vibali rasmi vya kufungisha ndoa takatifu kanisani hapo, ambao ni Askofu Mkuu na Askofu Msaidizi.

Kwa sasa, Askofu Msaidizi ni mama mzazi wa Askofu Mnai aitwaye Upendo Mnai ambaye  alifungisha ndoa hiyo ya kwanza Jumapili iliyopita tangu awe askofu msaidizi, huku kukiwa na mahudhurio ya waumini wengi, wakiwamo ndugu, jamaa na marafiki wa maharusi.

Mvuto wa ndoa hiyo ya Askofu haukuwa kanisani tu, bali ulianzia wakati wa maandalizi, kwani tofauti na yalivyo mazoea ya kuona bibi harusi mtarajiwa akiandaliwa sherehe ya 'Kitchen Party’ na upande wake, hali ilikuwa tofauti kwa ndoa ya Askofu Mnai, kwani mama mkwe wa bibi harusi mtarajiwa, Gloria Kaserwa ndiye aliyeandaa shughuli hiyo kwa ajili ya binti anayetarajiwa kuolewa na mwanawe.

Aidha, licha ya kuwa Askofu, Mnai katika kipindi chote cha maandalizi ya ndoa yake, alikuwa akihudhuria mafunzo maalumu ya ndoa kutoka kwa mchungaji wake.

Siku ya harusi yake, Askofu Mnai aliyezaliwa miaka 30 iliyopita aliingia kanisani na  kupokelewa kwa hoi hoi, nderemo na vifijo majira ya saa 9.00 alasiri na ilipotimu saa 11, ndoa  ilifungishwa rasmi na Askofu Msaidizi yaani mama yake mzazi.

Mara baada ya tukio hilo, wanandoa na wageni waalikwa walihudhuria sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Mwika iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam.

Wakati akiendesha ibada hiyo Mama Askofu Upendo, alisema: “Ndoa takatifu ina kibali mbele za Mungu, ndoa ni kitu endelevu, kila siku unajifunza kama shule inavyotaka, lakini leo tunashukuru tunahitimisha uchumba ili wapate baraka za kuwa mwili mmoja.”

Aliongeza kuwa, hesabu ya Mungu si kama ya wanadamu bali kwa Mungu moja na moja ni moja wala si mbili, kama kawaida ya hesabu tulizozizoea.

Alisema mwanaume ni kichwa cha nyumba, lakini hapaswi kuwa dikteta na kwamba kama akiwa hivyo, huyo hawezi kuwa kichwa cha nyumba tena, bali Simba, huku akionya kuwa,  'ubabe’ ndio unaosababisha ndoa nyingi kuwa na matatizo na hatimaye kuvunjika.

“Mungu amekutafutia mwanamke wa kufanana naye tabia na kuacha za awali kutoka kwa wazazi, sasa mwanaume kuwa ukiwa dikteta mkeo atakuwa hana likizo kwa mkubwa wake wewe, kumdharau ni kinyume cha mpango wa Mungu kwa kuwa huko si kufanana.”

Alisisitiza kwa maharusi hao kuwa kuolewa kuna raha sana kwa kuwa walioshibana kwa dhati na wanakuwa mithili ya watu wanaoishi peponi.

Mama Mnai alimsisitizia mkwe wake kumtii na kumpenda mume wake, akisema asipofanya  hivyo na kumtii, huenda akatoa mwanya kwa shetani kupata nafasi ya kuharibu ndoa na  kuzisambaratisha.

Huku akishangiliwa mara kwa mara, alionya kwa kusema; “Msiwachokoze waume zenu wasije wakajaribiwa na matokeo yake ni nyumba nyingi kuvunjika na kusababisha matatizo makubwa kwa jamii kama hili la watoto wanaoishi katika mazingira magumu, yaani chokoraa.”

Mmoja wa mashuhuda wa ndoa hiyo, Michael Sebastian (29) mkazi wa Temeke ambaye pia ni muumini kanisani hapo aliizungumzia ndoa hiyo kwa kusema: “Kwanza sijawahi kuona mafunzo ya maadili ya ndoa kwa mwanamke yakifundishwa na upande wa wakwe wa mwanamke.

“Na hata hili la mama kufungisha ndoa mwanawe wa kwanza kumzaa limenifurahisha na halitanitoka akilini mwangu, kwani kwangu ni moja ya maajabu ambayo nimezoea kuyaona kanisani hapa tangu nilipoamua kuokoka katika kanisa hili.”

Naye Mchungaji wa uchumba na ndoa, Peter Mwasandube alisema ilikuwa ni kitu cha  kumfurahisha sana na kuona anahitimisha harusi ya Askofu wake Mkuu kwani wakati wote  wa uchumba wao yeye ndiye alihusika kwa jambo lolote wakati wowote.

“Kwa hiyo sasa naona nitapumzika kidogo kwa kulifanikisha hili leo,” alisema. Kwa upande wa askofu Mnai na mkewe Gloria, waliahidi kuishi kwa maadili yanayopendeza duniani na mbinguni kwa msaada wa Mungu.

Alipoulizwa na mwandishi anajisikiaje baada ya kufungisha ndoa hiyo, Mama Mnai alisema,  “Kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza, nimemaliza kazi ambayo ilikuwa ngumu kabla ya kuifanya.”
Source: Habari Leo

Ni Sioi Sumari Arumeru...


MGOMBEA wa CCM uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, kutangaza uteuzi huo wa Kamati Kuu ya CCM
Sioi akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arumeru alipopita Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam leo muda mfupi baada ya CCM kumtangaza kuwa mgombea wake baada ya uamuzi wa Kamati Kuu jana
----
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemteua rasmi Sioi Sumari (pichani) kuwa mgombea wake wa  ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.

Akitangaza hatua hiyo,janajioni, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema  uteuzi huo umefanywa na  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, katika kikao chake kilichofanyika jana mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

Nape alisema, imesema CCM ina uhakika Sioi ataipeperusha vyema bendera ya CCM kwenye uchaguzi huo na bila shaka CCM itaibuka na ushindi baada ya uchaguzi utakaofanyika Aprili mosi mwaka huu.

Alisema, wakati siku ya uzinduzi wa kampeni za CCM utapangwa na Kamati ya kampeni ya mkoa wa Arusha na wilaya ya Arumeru, Kamati Kuu imemteua Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kufungua kampeni hizo.

Nape alisema, wakati mfumo mzima wa kampeni kwa jumla utaratibiwa na mkoa husika, kitaifa kampeni hizo zitaratibiwa na  Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye ndiye alikuwa pia Mratibu wa Kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Igunga mkoani Tabora ambako CCM iliibuka na ushindi.

Uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Sumari ambaye ni baba mzazi wa mgombea wa CCM Sioi.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kampeni jimboni humo zitaanza rasmi tarehe tisa mwezi huu ambapo vyama vya CCM na CHADEMA vinatarajiwa kuonyeshana umahiri wao katika kampeni hivyo kwa kuwa ndivyo vyama pekee vinavyoonyesha kuwa na ushindani wa kutosha.

Sioi amefanikiwa kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM, baada ya kupita katika tanuru kali la mchakato wa kura za maoni jimboni kwake ambapo mara ya kwanza alishinda lakini uchaguzi ukalazimika kurudiwa kwa maagizo ya Kamati Kuu ya CCM baada ya yeye na mshindani wake wa karibu, Srakikya kupata kura zisizovuka asilimia 50 ya kura zote.

Uchaguzi wa marudio ulifanyika jana, kwa kuwapambanisha Sioi na Sarakikya tu, na hatimaye Sioi akaibuka mshindi kwa kura zilizozidi asilimia 50, hatua iliyofuatiwa na jina lake kupelekwa Kamati ya wilaya na mkoa wa mapendekezo kabla ya jina lake kutinga kamati kuu jana

Saturday, March 3, 2012

SERIKALI YAAGIZA MISHAHARA YA TAZARA ILIPWE HARAKA


Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)jana katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa TAZARA umekuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo
Baadhi ya watendaji wakuu wa wizara ya Uchukuzi wakimsikiliza Waziri Omari Nundu (hayupo pichani) wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)jana jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa TAZARA umekuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Omari Chambo.
Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) tawi la TAZARA wakijadili mambo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utendaji kazi wa Mamlaka ya TAZARA baina ya Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu na waandishi wa habari uliofanyika jana  jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa Mamlaka hiyo umekuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo.Kutoka kulia ni Lufingo Mwanghba, Bundala Kabulwa, Yassin Mleke na Benjamini Kehogo.
---- 
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
SERIKALI imeigiza menejimenti ya TAZARA kuhakikisha kwamba mishahara ya wafanyakazi wake inalipwa haraka.
Aidha imeongeza kuwa menejimeti hiyo ihakikishe yanapotokea matatizo inayashughulikia na kutoa maamuzi kwa muda muafaka.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo(jana) jijini Dares Salaam kuhusu utendaji kazi wa TAZARA.
“Changamoto zilizopo hivi sasa ni TAZARA kutoweza kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakati na kutokuwa na mafuta kwa ajili kuendesha treni za abiria . hadi jana kuna baadhi ya wafanyakazi hawakuwa wamelipwa mishahara ya Januari na Februari, mwaka 2010 na wote mishahara ya Februari hawajalipwa .
“Kutokana na hali hiyo wizara imeiagiza menejimenti ya TAZARA ihakikishe kwamba ifikapo Machi 2, 2012 mishahara ya Januari iwe imelipwa na mafuta yawe yamepatikana kwajili ya kuendesha angalau treni tano kwa siku. Mishahara ya Februari nayo ilipwe haraka,” alisema Waziri Nundu.
Aliongeza kuwa tayari menejimenti hiyo imekamilisha taratibu za kuingiza fedha za mishahara ya Januari katika benki, hivyo itawafikia wafanyakazi wa Mbeya Machi 3,mwaka huu na mishahara ya Februari ilipwe katikati ya Machi, mwaka huu.
Alifafanua kuwa tayari TAZARA imeshapata lita 600,000 za mafuta , hivyo leo treni nane zimeshanza kufanya kazi kati ya hizo za sita ni za mizigo.
Waziri Nundu alisema mikakati iliyopo sasa ni kuiongezea TAZARA uwezo wa uchukuzi kwa kukarabati injini na mabehewa yaliyopo, kuboresha miundombinu ya reli pamoja na njia za mawasiliano na kuendeleza ushirikiano mzuri wa wateja wakubwa katika kukarabati injini na mabehewa kwa makubaliano maalumu.
Alisema Baraza la Mwaziri la TAZARA limepanga kukutana Mei 23,mwaka huu kujadili masuala ya shirika hilo kwa kina zaidi na kupata ufumbuzi ili kuboresha huduma ziwe za kudumu.
Waziri Nundu aliongeza kuwa atakutana na wafanyakazi wa TAZARA Machi 23, mwaka huu na kukagua shughuli za utendaji kazi na njia ya reli kutoka Dares Salaam hadi Tunduma.

Friday, March 2, 2012

SHULE YA WAMA WAPATIWA MSAADA WA BASI LA SHULE, VITABU NA VIATU KUTOKA KWA ASBURY PARK SCHOOL DISTRICT YA NEW JERSEY NA NEW JERSEY NATURAL GAS


Mjasiriamali loveness Mamuya kisoma barua kutoka kwa first lady Mama Salma Kikwete.

Wanafunzi wakikabidhi viatu kwa Mamuya na shaban kutoka kwa mkurugenzi wa New Jersey Natural Gas.

Basi walilo zawadiwa kwa shule ya WAMA Tanzania. bus hili linauwezo wa  wanafunzi hamsini. 

Ndani ya School Bus walilo zawadiwa wanafunzi wa WAMA. Kwa picha zaidi bofya hapa

" Wee, Nani Kakuruhusu Unifotografu....!"


.... Usiondoke hapa mpaka uandike maelezo!

Thursday, March 1, 2012

Is Obama now so unpopular even this hopelessly gaffe-prone Mormon moneybags could topple him?



After a wild rollercoaster ride for the past two months since voting began in Iowa, Republicans can now calm down and look at the man who is overwhelmingly likely to be the candidate charged with unseating President Barack Obama in November.

It was neither easy nor pretty but Mitt Romney's narrow three-point victory in his native state of Michigan, the place where he was born, grew up and where his father was governor in the Sixties, puts him firmly in command over his main challenger Rick Santorum.

Three weeks ago Santorum stunned Romney and the party elders who back him, scoring wins in Colorado, Minnesota and Missouri, and then leaping to a 15-point poll lead in Michigan. Romney showed he had the determination, resilience and steely nerve to overcome a surging opponent at the moment it really mattered.

Under pressure: President Barack Obama's approval ratings are down and he is looking vulnerable Under pressure: President Barack Obama's approval ratings are down and he is looking vulnerable

Republican presidential candidate, former Massachusetts Governor Mitt Romney, speaks to supporters at his election watch party after winning the Michigan primary Republican presidential candidate, former Massachusetts Governor Mitt Romney, speaks to supporters at his election watch party after winning the Michigan primary

Having at times let their fevered imaginations dream up scenarios of a white knight such as Governor Chris Christie of New Jersey or Governor Mitch Daniels of Indiana entering the fray, Republicans are now looking at the reality of a Romney candidacy.

Talk of the first 'brokered convention' since the Forties — a convention where candidates are deadlocked — will now recede. Romney's double win in Michigan and Arizona, where he cruised home by 20 points, means that order is at hand.

On 'Super Tuesday' next week, when ten states vote, the former Massachusetts governor, venture capitalist, saviour of the 2002 Winter Olympics and Mormon is likely to seal the deal. Read more>>

AMB AMINA SALIM ALI in INVESTMENT drive for AFRICA


Ambassador Amina S. Ali, The African Union representative to the United States of America (third left) while mobilizing Investment in Africa from the United States as it was captured during a committee meeting in California recently. Included in the picture are the Presidents of African Chambers of Commerce and leading experts on trade and investment.

Mobile Clinics...


 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda(kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari   la huduma ya mkoba (mobile clinics) Dk. Noah Chihoma kutoka Hopitali ya  Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda(kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari   la huduma ya mkoba(mobile clinics)  mwakilishi wa hospitali ya Rufaa ya  Bungando, Neema Mshana.
baadhi ya watumishi wa afya wakiwemo waandishi wa habari wakimwangalia Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda wakati akiendesha mmoja ya gari  ya huduma ya mkoba(mobile clinics) .
Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo. 

 NA MAGRETH KINABO – MAELEZ0
1/3/2012
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa magari  saba  ya huduma  za mkoba  kwa ajili ya  kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma za madaktari bingwa hususan walioko vijijini.
Kauli  hiyo ilitolewa  leo (jana) na Waziri wa Afya na  Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda  wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi magari hayo kwa wawakilishi wa hospitali mbalimbali kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
“Tunagawa magari haya kwa madhumuni ya kupeleka huduma za wataalamu bingwa karibu na wananchi.
 “Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne ni kuhakikisha huduma za afya na ustawi wa jamii zinawafikia nchinii kote na hasa vijijini, ambako ndipo wanapoishi wananchi wengi. Haya magari yatatumiwa na madaktari bingwa katika kanda zetu zote nchini kote,” alisema Waziri Mponda.
  Aliitaja thamani ya magari hayo kuwa ni sh. milioni 181 kwa kila mmoja ambayo inahusisha pamoja na vifaa vilivyoko ndani ya gari.
Waziri Mponda aliongeza kuwa watumishi kutoka hospitali husika watafundishwa namna ya kutumia magari hayo ambayo yana vifaa maalaum vipya vya kisasa, ambao watawaelekeza wenzao wakati wa kliniki hiyo.
 Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vya kufanyia uchunguzi na vya kutolea huduma. Magari hayo pia yana jenereta kwa ajili ya kupata umeme sehemu ambazo hazitakuwa na umeme.  
 Hospitali zilizopata magari hayo  za Kanda ya Mashariki ni CCBRT  Dares Salaam, Kasikazini  KCMC  Kilimanjaro, Kati  Chuo Kikuu cha Dodoma Kusini  Rufaa ya Mbeya, Kusini Mashariki Ndanda Mtwara, Magharibi Maweni Kigoma na Ziwa Bugando.
Wakizungumzia kuhusu magari hayo wawakilishi wa hospitali hizo walisema wanaishukuru  serikali kwa kuwa utawezesha wananchi wasioweza kufikia huduma za afya kuzipata kwa kiurahisi.

Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB)Amtembelea Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Bibi Tonia
Kandiero,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,kujitambulisha kwa Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Bibi Tonia Kandiero,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,kujitambulisha kwa Rais.Picha na Ramadhan Othaman,IKULU-Zanzibar

SINTAH:MAGUBE GUBE FAKE YA KIMASAI NDANI YA ZANZIBAR

MAGUBE GUBE FAKE YA KIMASAI NDANI YA ZA

maana kuna wengine hawakawii
kusema sikuwepo
siku hizi ni kimya kimya tuu mwendo
mzima

NZIBAR


maana kuna wengine hawakawii
kusema sikuwepo
siku hizi ni kimya kimya tuu mwendo
mzima





Hallows

ngoja niwape mkasa wa weekend iliyopita ndani ya  znz

mmmh nilikuwa katika hotel yenye hadhi ya kimataifa Melia, hapo zamani ilikuwa inaitwa Kempiski.

basi kwa pembeni yake kukawa kuna disco la beach vile nikasema ngoja nijitupe na washikaji zangu,looh asalalee naingia naona rangi nyeupe nyingi sana(whites)weusi mbali na company yangu,wahudumu waliobaki ni wale wazee wakuruka juu(Masaiii)duuh nikajiuliza inakuwaje??

hahaaa kumbe si wamasai,ni watu wanaojifanya  wamasai eti na kusuka kabisa,hawa vijana wanatumika kule kwaajili ya shughuli za ngono,duu si wanawake tuu katika mtanange huu
yaani wazungu wakija wanawadaka na siunajua tena wazungu kuna vitu wanapenda kutoka bara hili,yaani wamasai fake wanaweza hata kuuana kisa nani apate mama mwenye pension kubwa,yaani ni style fulani  kama ya madada poa.

wale tours,na nk please watahadharisheni wageni wenu wanaoenda znz wale si wamasai bali wana act,na serekali ya znz jamani ifanye kitu kuhusiana na hilo maana its so nasty jamani natamani ungekuwepo arrrgh.


PARTY ILIANZA HIVI WATU PIPO FULL KUJIACHIA MCHANGANI NA UKILEWA KAJITUPE BAHARINI UZINDUKE TENA


mmmh hivi vitu ndo ninavyopenda mimi
ku party mbali,hamna anayekujua
full kujiachia


si umeona mwenyewe ki beach beach
watu wanajiachia mbaya hela nyie acha tuu




huyooo mlengwa jamani
maana nili zoom kutoka mbali
eti huyu ndie mkewe


maana kuna wengine hawakawii
kusema sikuwepo
siku hizi ni kimya kimya tuu mwendo
mzima

MCHEZAJI WA ZAMANI WA TIMU YA TANZANIA PRISONS AJINYONGA KWA KAMBA, MWENYEKITI WA KIJIJI AVULIWA MADARAKA NA RAIA WAKE - MBEYA



Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.

Mtu mmoja aitwaye Gesho Brown(37), mkazi wa Kitongoji cha Pipe Line mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani Mbeya amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba.

Mwili wa marehemu Gesho ambaye pia amewahi kuichezea timu ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya, uligunduliwa na shemeji yake aitwaye Bahati majira ya saa 5 kamili asubuhi na kutoa taarifa kwa mjumbe wa eneo hilo aitwaye Bi Edda Yusto ambaye naye alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa.

Mara baada ya taarifa kumfikia Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Asifiwe Mwakalonge alitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mbalizi ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika Hospitali ya Ifisi kwa uchunguzi.

Hata hivyo sababu za kifo chake hazijabainishwa na marehemu alikuwa akiishi pekee yake nyumbani.

Wakati huo huo wananchi wa kijiji cha Sheyo kata ya Ibaba wilaya ya Ileje wamemwachisha uongozi Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Denison Simbeye pamoja na serikali yake baada ya tuhuma za wizi wa ng’ombe wa kijiji wenye thamani zaidi ya shilingi laki tatu za kitanzania.

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa hadhara ulioanza majira ya saa nne asubuhi na kumalizika saa 11 jioni ambapo mkutano uliazimiwa na mwenyekiti huyo na serikali yake wachukuliwe hatua za kisheria.

Katika mkutano huo wananchi waliwasimika Bwana Reuben Shibanda na wenzake kuchukua nafasi zilizoachwa wazi na viongozi waliondolewa kutokana na ubadhilifu.

Habari hii kwa hisani ya Chimbukoletu.Blog

Wednesday, February 29, 2012

Allan Lucky of "Skongaaa" got Married to Haika Samwel


 The two love birds making their vows to each other...
 And there came the moment...
 Allan and Haika exchanged rings to form one family...

 The family and friends witnesses to this beautiful union!!
 Dont they just look amazing!! I love the colors..yellow and white look superb!!
 Aaaaaw!! my mouth waters!! thats a good looking cake!! I hope my part is still in your fridge,Allan!
 And now...you can kiss the bride!! Ladies and gentlemen, i bring Mr. and Mrs. Allan Lucky Komba!! I wish you guys the best of luck in your new life... Stay blessed always!!

 And special congrats to you, Allan.....the Students' President of Tanzania..lol


xoxo
Missie Popular

Baraza la Vijana wa CHADEMA Linakaribisha Maombi ya Kushiriki Mafunzo ya Wanasiasa Vijana Nchini Ujerumani


Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limekuwa na kawaida ya kutoa fursa za mafunzo ya makada wake ndani na nje ya Tanzania.

Dira ya BAVICHA ni kuona vijana ni nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa maendeleo yao na ya taifa.
Kwa awamu hii BAVICHA limepanga kupeleka kada wake kwenye mafunzo ya wiki moja kwa wanasiasa vijana (Summer School) Berlin, nchini Ujerumani.

BAVICHA inawaalika vijana wa CHADEMA watakaopenda kushiriki mafunzo hayo kutuma barua ya maombi ya kushiriki, ikiambatana na wasifu unaojitosheleza (CV).

BAVICHA inahimiza vijana kutuma maombi kwa kuwa taarifa za waombaji zitahifadhiwa katika kumbukumbu (data bank) kwa ajili ya fursa nyingine zinazojitokeza.

Mwombaji pia anatakiwa ataje mawasiliano yake, namba ya kadi yake ya uanachama, tarehe ya kujiunga na chama na aeleze ushiriki wake ndani ya BAVICHA na Chama pamoja na matarajio yake ndani ya BAVICHA na CHADEMA kwa ujumla.

Maombi yatumwe kwa 
Katibu Mkuu wa BAVICHA kupitia
kabla ya tarehe 10/03/2012.

The Prime Minister Mizengo Pinda Speaks to Prof. Paul Collier From Oxford University the the United Kingdom

The Prime Minister , Mizengo Pinda speaks to Prof. Paul Collier  (left) from Oxford University the the United Kingdom after opening of the  Round table  Discussions amongst the senior Leaders on Managing Natural Resources to  Ensure Prosperity in Africa at  Hyatt Regency- Kilimanjaro Hotel in Dar es salaam on Feb, 28,2012.
The Prime Minister Mizengo Pinda speaks to participants   after  openingof the  Round table  Discussions amongst the senior Leaders on Managing Natural Resources to  Ensure Prosperity in Africa at  Hyatt Regency- Kilimanjaro Hotel in Dar es salaam on Feb, 28,2012.Photo By Prime Ministers's Ofice

President Jakaya Mrisho Kikwete launching the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment Programme (CSRE)


President Jakaya Mrisho Kikwete speaks  last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam
President Jakaya Mrisho kikwete greets the chairman of Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Judge Mark Bomani (rtd) last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam. Looking on is ambassador Juma Mwapachu.
President Jakaya Mrisho Kikwete arrives last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam. Right is the British High Commissioner to Tanzania Ms Diane-Louise Corner, second left is the Minister for minerals and Energy Mr William Ngeleja and far left is the Dar es salaam Regional Commissioner Mr Meck Sadik.
President Jakaya Mrisho Kikwete arrives last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam. Right is the Minister for minerals and Energy Mr William Ngeleja and left is the Dar es salaam Regional Commissioner Mr Meck Sadik.Photo By State House
--
SPEECH BY HIS EXCELLENCY DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLICOF TANZANIA, AT THE LAUNCHING OF THE PRESIDENTIAL AWARD ON THE EXTRACTIVE INDUSTRY CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITIES AND EMPOWERMENT (CSRE) HELD AT HYATT KILIMANJARO HOTEL ON 28th FEBRUARY, 2012

Hon. William Ngeleja, Minister for Energy and Minerals;
Hon. Ministers, Deputy Ministers,
Hon. Regional Commissioners;
Hon. Members of Parliament;
Ambassadors and High Commissioners;
Mr. Joseph Kahama, President of the Tanzania Chamber of Energy and Minerals;
Ms. Catherine Lyombe, Mining Stakeholders Forum;
Invited CEOs of Extractive Companies and Related Services; Representatives of Financial Institutions;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;

I thank you honourable Minister for inviting me to participate at this historic event of launching the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment Programme (CSRE). I am delighted that the Award will be contested annually and companies with outstanding performance will be acknowledged.  

Ladies and Gentlemen;
I am happy with the key indicators developed to evaluate the scores for the Award.  In this regard, I consider very pertinent indeed, to include in the indicators things like;
1.     Community well-being and sustainability;
2.     Human resource development and training;
3.     Local industry participation;
4.     Community safety, water and environment;
5.     Social infrastructure such as housing and health services; and,
6.     Infrastructure development such as roads, electricity etc.

I commend you, and all those involved in conceiving the ideas and all those who made it happen as we are witnessing today.  
The Presidential Award on CSR and Empowerment that we are launching tonight is an important milestone in the history of the extractive industry in Tanzania.  It is intended to align corporate policies and practices of companies in the extractive industry with sustainable development.  It is about making local communities where companies operate, benefit from the operations of the companies.    And, it is about the companies benefitting from the friendliness, harmony, understanding and cooperation that will ensue with the government and the people in the areas where the companies operate. 

Business leaders;
Ladies and Gentlemen;
The concept of CSR is not new to Tanzania, the world and to all of us gathered here this evening.  Nowadays, it is increasingly becoming a normal international practice.  Almost all major companies in the country have put corporate social responsibility in their mission statements, policies and internal management systems.  What is new to us Tanzania, therefore, is the Award we are launching tonight.  Otherwise, companies have been working to ensure that local communities receive some direct benefits, and contribute to broadening social and economic sustainable development.

If principles of Corporate Social responsibility are observed and delivered, companies will enjoy very good relations with the communities around them.  If companies pay taxes that are due to the State, rightfully and timely, they will have good relations with the government.  Likewise, if the government and communities aptly deliver on their part of the responsibilities they will enjoy good relations with companies.  In the end everybody benefits and a win-win situation will be realised.  I believe, this is the best insurance policy one can long to have as an investor and as an investment destination.  If this is absent there is every risk of friction which is not healthy for business and may put the investment in jeopardy.  Everybody will be at risk losing.

Ladies and Gentlemen;
As alluded to earlier, under CSR and Empowerment, companies are expected to contribute to the provision of important social and economic services to the communities where companies are located.  Besides that, I would like to mention and underscore two or three importance things.  The first one is about sourcing goods and services locally.  Companies should make it their policy to engage local companies and local people in this regard.  There are services which can be sourced locally, there is no need of importing them from abroad.  This is the best way to promote local empowerment and an excellent way of promoting socio-economic growth in the economy of the area and the country.  

This way, the company is integrating itself in the socio-economic life of the people by creating jobs and incomes.  It engenders, what economists call backward and forward linkages.  This will make the people strongly feel a sense of ownership and an obligation to protect the investment.  But if such things are absent people will have no stake in operations of the company.  As a result, they may care less about the presence, survival and progress of the company.  They may even turn hostile.  May I make a humble appeal to all companies in different sectors to take this matter seriously. 

The other thing I would like to mention with regard to CSR policies is the relationship between large companies and small companies and local people engaged in the same industry.  It is incumbent upon large companies to realise that assisting local players to make progress is in their best interest.  

Big companies should use their economic strength and technological capacity to help small players improve their operating systems, increase productivity, production and improve their affairs in general.  I believe, it will reduce jealousies, minimise friction, avoid unnecessary hostility and increase friendship and cooperation.  Take the case of artisanal mining activities in the vicinity of large mining operations in Tanzania.  If the latter assists the former and treat each other as partners, instead of competitors or contenders, it will very much improve relations between the two players who need each other.  It will clear undue misunderstanding and remove the mistrust and resentment.  Attitudes of hostility, threats and violence can easily be avoided.  In the end everybody benefits.  

Ladies and Gentlemen;
The extractive industry can emulate the good practice of out-growers scheme around sugar plantations and sugar factories in Tanzania. In those cases, the large company supports small scale farmers, as out-growers, in several ways including provision of important services such as extension services, seedlings, technical know-how and market for their sugar cane.  I think this is a good model to look into.  It enhances local productive capacity and ensures sustainability of income to farmers. May this Award inspire companies in the extractive industry to emulate this example and strive to do what is possible to assist the local small scale investors grow and promote long-term economic and social sustainability.

Ladies and Gentlemen;
We in government consider CSR and Empowerment in the extractive industry very important indeed.  By their very nature, most of the operations in extractive industry are not renewable.  They get depleted as extraction continues.  As such if there are no proper arrangements for tangible benefits to the communities where the operations are located, they could easily become a source of discontent and resentment.  When the resources are completely exhausted and operations are stopped, the questions people would hasten to ask is about how did they benefit? The centrality of having mechanisms whereby communities and the country benefits even at the end of the life of the operations, therefore, need no emphasis.  

We would like to see when such eventuality comes, everybody says we have benefited.  Contrary to that may create apprehensions and even resentment of large investors in the extractive industry especially when they are foreign based.  I believe, this is doable.    Let us heed the old adage “where there is will there is a way”.   Let us gunner the will to do it for our sake.
Honourable Minister;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;

Before I conclude, let me, once again, sincerely thank the Mining Inter stakeholders’ Forum (MISF) and the Ministry of Energy and Minerals for conceiving the idea and introducing the CSRE Presidential Award in Tanzania. We are a little bit late, but it is better late than never. 

I am confident the Award will stimulate and encourage the extractive companies to take interest in the communities around them and deliver on corporate social responsibility and empowerment. I invite business leaders here tonight to heed this our call and rise to the challenge. 

With these many words, I now announce that the Corporate Social Responsibilities and Empowerment Presidential Award on Extractive Industry is officially launched.
Thank you for your kind attention!